Rais wa Klabu ya Yanga SC na Mwenyekiti wa Chama cha Vilabu Afrika (ACA), Eng. Hersi Said, ameandika historia mpya baada ya kuteuliwa rasmi na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Vilabu ya Wanaume Duniani kwa kipindi cha miaka minne (2025–2029).
Kwa uteuzi huu, Eng. Hersi anakuwa mtu wa kwanza kutoka Afrika Mashariki na Kati kuingia katika moja ya kamati kubwa na zenye ushawishi mkubwa ndani ya FIFA, hatua inayodhihirisha kuaminika kwake kimataifa na mchango wake katika maendeleo ya soka barani Afrika.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Kwa mujibu wa barua rasmi ya FIFA iliyotiwa saini na Naibu Katibu Mkuu, Mattias Grafström, uteuzi huo unazingatia kanuni za FIFA na taratibu za utawala bora. Eng. Hersi Said anatarajiwa kupokea maelekezo ya awali kupitia barua pepe ili kurasimisha taarifa zake binafsi kwa ajili ya kuanza rasmi majukumu yake.
Uteuzi huu ni ishara ya kuongezeka kwa ushawishi wa viongozi wa soka wa Afrika Mashariki katika meza za maamuzi ya kimataifa, na unatarajiwa kufungua milango zaidi kwa maendeleo ya vilabu vya kanda hii.