Jeanine Afungiwa Na Tff Kisa  Sintofahamu Ya Jinsia

Baada ya taarifa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwamba limemsimamisha kwa muda mchezaji wa klabu ya Yanga Queens, Princess Jeanine Mukandiyisenga, raia wa Rwanda, kupisha uchunguzi wa kina kuhusu jinsia yake, mambo mapya yamezuka.

Hatua hii ilikuja baada ya sintofahamu kuibuka mitandaoni na katika baadhi ya duru za michezo, ambapo mashabiki na wadau walianza kuhoji hali halisi ya jinsia ya mchezaji huyo, ambaye amekuwa akionesha kiwango cha juu mno katika michezo ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.

Jeanine Afungiwa Na Tff Kisa  Sintofahamu Ya Jinsia

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya TFF, uchunguzi huo unalenga kuthibitisha ukweli bila upendeleo, kwa mujibu wa kanuni za shirikisho hilo na taratibu za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuhusu wachezaji wa kike. Kwa sasa, Jeanine atabaki nje ya kikosi cha Yanga Princess hadi uchunguzi utakapokamilika na taarifa rasmi kutolewa.

TFF imewataka mashabiki na wadau wote wa soka kuwa watulivu na kuepuka kutoa maoni ya kudhalilisha au ya kibaguzi, ikisisitiza kuwa mchakato huu ni wa kawaida na wa kisheria katika michezo ya kimataifa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Jeanine Afungiwa Na Tff Kisa  Sintofahamu Ya Jinsia

Wakati habari hiyo ikiwa bado imetengeneza maswali mengi, mchezaji huyo ameibuka na kudai kuwa kinachoendelea ni chuki, wivu  na uoga tu wa wapinzani wao Simba Queens.

Jeanine alisema: “Najua hii ni chuki na uoga tu, wanahofu nitawafunga, kwa sababu mimi ni mkali. Nacheza timu ya taifa ya Rwanda.

“Nimecheza ligi ya wanawake ya Rwanda na msimu uliopita pia nilicheza hapa. Kwanini itokee loe. Mimi ni mwanamke na kinachoendelea ni chuki na wivu.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.