Katika taarifa iliyotolewa na Marca, La Liga ilithibitisha kuwa mashabiki wa Atletico Madrid na Real Madrid walijihusisha na tabia isiyofaa. Mashabiki wa Atlético waliripotiwa kuwatukana mara kwa mara wachezaji wa Real Madrid na mashabiki wao waliokuwa wamesafiri hadi Metropolitano. Kwa upande mwingine, baadhi ya mashabiki wa Real Madrid walimlenga kocha wa Atlético, Diego Simeone, kwa matusi ya moja kwa moja.
Ripoti hiyo ya La Liga iliorodhesha matukio matano ya mashabiki wa nyumbani, yakiwemo kurusha kitu kutoka jukwaani (ambacho kwa bahati hakikumjeruhi mtu yeyote) na nyimbo za matusi. Vilevile, mashabiki wa ugenini walinaswa wakitoa matusi kwa Atlético, klabu yao na kocha Simeone katika matukio matano tofauti.
Lakini Madrid derby haikuwa mechi pekee iliyochunguzwa. Katika mechi ya Girona dhidi ya Espanyol, mashabiki wa nyumbani waliripotiwa kuwatukana wageni mara tatu, huku mashabiki wa Espanyol wakiripotiwa kuwatukana Girona na hata Barcelona. Mechi ya Getafe dhidi ya Levante pia haikuachwa, refa alitukanwa mara mbili na mashabiki wa nyumbani.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
La Liga inaendeleza juhudi za kukabiliana na tabia hizi kupitia jukwaa lake la LALIGAVS, ambalo linawapa mashabiki nafasi ya kuripoti matukio ya vurugu na matusi moja kwa moja kutoka viwanjani. Hii ni sehemu ya kampeni ya muda mrefu ya La Liga kutaka mamlaka zaidi ya kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika.
Kwa kuzingatia ukubwa wa mechi kama Madrid derby, na athari zake kwa taswira ya soka la Uhispania, presha inaongezeka kwa La Liga kuhakikisha viwanja vinabaki kuwa salama, vya heshima na vya burudani kwa mashabiki wote