Amorim Njia Panda Man United, Southgate Kuwa Mrithi

Kocha wa Manchester United, Ruben Amorim, anakabiliwa na presha kubwa baada ya kikosi chake kushuka hadi nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Premier League kufuatia kipigo cha 3-1 dhidi ya Brentford. Licha ya ushindi wa morali dhidi ya Chelsea siku chache kabla, United walionekana kupoteza mwelekeo kabisa kwenye uwanja wa Gtech Community Stadium.

Benjamin Sesko alifunga bao lake la kwanza akiwa na United, lakini juhudi zake ziligubikwa na udhaifu wa kikosi kilichoruhusu mabao mawili ndani ya dakika 20 za kwanza, na cha tatu katika dakika za majeruhi. Matokeo hayo yamewaacha mashabiki wakihofia kurejea kwa hali ya msimu uliopita, kutokuwa na mwelekeo, kukosa ubunifu, na matokeo yasiyoridhisha.

Amorim Njia Panda Man United, Southgate Kuwa Mrithi

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Goal na Sports Mole, Manchester United wanatazama kwa makini tarehe 1 Novemba, ambapo fidia ya kumfuta kazi Amorim itapungua kwa kiasi kikubwa. Hii imezua tetesi kuwa klabu inaweza kusubiri hadi tarehe hiyo kabla ya kufanya maamuzi rasmi.

Sir Jim Ratcliffe, mmiliki mwenza wa United kupitia kampuni ya INEOS, anaripotiwa kuwa na nia ya kumleta Gareth Southgate kama kocha mpya. Southgate, ambaye aliongoza England kufika fainali za Euro 2020 na Euro 2024, yuko huru tangu alipojiuzulu baada ya mashindano ya Ulaya mwaka huu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Amorim Njia Panda Man United, Southgate Kuwa Mrithi

Majina mengine yanayozungumzwa kuwa mbadala wa Amorim ni Oliver Glasner wa Crystal Palace na Andoni Iraola wa Bournemouth, lakini Southgate anaonekana kuwa chaguo la karibu zaidi kutokana na uhusiano wake wa muda mrefu na Ratcliffe.

Mashabiki wa United wameonyesha hasira baada ya tukio la Brentford kuepuka kadi nyekundu katika mechi hiyo, jambo lililozua mjadala mkubwa. Hata mwamuzi wa zamani wa EPL, Mark Halsey, alikosoa uamuzi huo, akisema ulikuwa na athari kwa matokeo ya mchezo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.