Napoli wameipa Galatasaray tarehe ya mwisho ya kuwasilisha nyaraka zote muhimu za usajili wa Victor Osimhen, baada ya pande zote mbili kukubaliana kuhusu kipengele kinachozuia uhamisho kwenda klabu nyingine za Serie A na masuala ya mgao wa asilimia ya mauzo ya baadaye.

Majadiliano haya yamechukua muda mrefu majira haya ya kiangazi, baada ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Nigeria kutumia msimu uliopita kwa mkopo Galatasaray, ambako alifunga mabao 37 katika mechi 41 rasmi na kutoa pasi za mabao 8.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
Ingawa mkataba upo karibu kukamilika, Napoli hawako tayari kusubiri milele. Subira yao imepungua, na sasa wameweka tarehe ya mwisho kuwa Jumatatu, wakiamini kuwa Galatasaray ina muda wa kutosha kukamilisha nyaraka zote zinazohitajika.
Masuala magumu tayari yameafikiwa €40 milioni italipwa papo hapo, €35 milioni zitalipwa kwa awamu hadi kufikia Juni 2026.



 
 
 
 
 
 
 
