Simba Wanautaka Ubingwa Kwa Kila Namna

Simba SC imeendelea kuonyesha makali yake katika Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/26 kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Namungo FC, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 1, 2025. Ushindi huo umewaweka kileleni kwa pointi 6, sawa na Singida Black Stars, lakini wakiwa na uwiano bora wa mabao.

Katika mchezo huo, Chamou Karabou alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 43 kwa kutumia pasi ya kona kutoka kwa Joshua Mutale. Bao la pili lilifungwa na beki mpya Rushine De Reuck dakika ya 60, akimalizia faulo ya Maema kwa ustadi mkubwa. Seleman Mwalimu alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la tatu dakika ya 84.

Simba Wanautaka Ubingwa Kwa Kila Namna

Rushine De Reuck, raia wa Afrika Kusini, ameweka rekodi ya kipekee kwa kuwa beki wa kwanza msimu huu kufunga mabao katika mechi mbili mfululizo. Wiki iliyopita, alifunga bao lake la kwanza dhidi ya Fountain Gate FC kwa kumalizia kona, na sasa amerudia tukio hilo dhidi ya Namungo FC.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Kutokana na mchango wake mkubwa, Rushine alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi, na hiyo ikawa tuzo yake ya kwanza tangu aanze kucheza soka Tanzania. Uwepo wake umeongeza nguvu katika safu ya ulinzi ya Simba, huku pia akionyesha uwezo wa kuchangia kwenye mashambulizi.

Simba Wanautaka Ubingwa Kwa Kila Namna

Kwa sasa, Simba SC inaonekana kuwa na muunganiko mzuri wa kikosi, huku wachezaji wapya wakianza kung’ara mapema. Mashabiki wa Msimbazi wana kila sababu ya kutabasamu, wakitazamia msimu wenye mafanikio makubwa.

Makala ijayo

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.