Kocha mpya wa Raja Casablanca, Fadlu Davids, ameanza rasmi safari yake ya ukocha nchini Morocco kwa ushindi wa kuvutia ugenini dhidi ya Difaâ El Jadidi, katika mechi ya tatu ya Ligi Kuu ya Morocco (Botola Pro). Ushindi huo wa bao 1-0 si tu umeweka alama ya mwanzo mzuri kwa Fadlu, bali pia umeisogeza Raja hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
Baada ya raundi tatu za mwanzo, Raja Casablanca na MAS Fez wote wameshinda mechi mbili na kutoa sare moja, wakikusanya alama 7. Cha kuvutia zaidi, timu zote mbili zimefunga mabao 4 na hawajaruhusu bao lolote, rekodi safi ya ulinzi inayowapa hadhi ya kuwa miongoni mwa wagombea wa ubingwa msimu huu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Fadlu Davids, ambaye aliiongoza Simba SC kwa mafanikio kabla ya kujiunga na Raja, ameanza kuonyesha athari zake mapema. Safu ya ulinzi ya Raja imeimarika, huku kikosi kikicheza kwa nidhamu na kasi ya juu. Wachambuzi wa soka nchini Morocco wanasema Davids ameleta falsafa mpya ya mpira wa kushambulia kwa akili, huku akitumia wachezaji chipukizi kwa ufanisi mkubwa.
Raja Casablanca sasa inajiandaa kwa mtanange wa nyumbani dhidi ya FUS Rabat wikiendi hii, mechi inayotazamiwa kuwa kipimo kingine cha uwezo wa Davids na kikosi chake. Mashabiki wa Raja wameonyesha matumaini makubwa, wakiamini kuwa msimu huu unaweza kuwa wa kurudisha heshima ya klabu hiyo kwenye soka la Afrika.