Licha ya tetesi zinazozagaa mitandaoni na kwenye vijiwe vya soka kuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC, Roman Folz, huenda akatupiwa virago, taarifa za ndani kutoka kwa mabosi wa klabu hiyo zinathibitisha kuwa hakuna mpango wa kuachana naye kwa sasa.
Yanga SC, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara ya NBC msimu wa 2025/26, wamecheza mechi mbili tu hadi sasa, dakika 180 za ushindani. Walianza kampeni yao kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Pamba Jiji FC katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, kabla ya kulazimishwa sare tasa na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine mnamo Septemba 30, 2025.
Sare hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Folz msimu huu, lakini haijatosha kutikisa nafasi yake. Viongozi wa Yanga wameripotiwa kuendelea na mazungumzo ya ndani na kocha huyo, wakitathmini mwenendo wa timu na kutafuta njia za kuboresha pale palipoonekana changamoto.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Katika hali ya kuvutia, watani wa jadi Simba SC nao wanakabiliwa na sintofahamu ya benchi la ufundi, kwani hadi sasa hawajamtangaza kocha mkuu. Hali hii imeongeza joto la ushindani wa nje ya uwanja, huku mashabiki wakisubiri kuona nani ataimarika zaidi kabla ya mechi za watani wa jadi.
Kwa sasa, Roman Folz bado yupo yupo sana Jangwani na inaonekana Yanga SC wanamtazama kama sehemu ya mpango wao wa muda mrefu, si tu kwa matokeo ya haraka bali kwa uthabiti wa kiufundi.