Ibenge Atoa Neno  La Matumaini Azam Fc

Kocha mkuu wa Azam FC, raia wa DR Congo, Florent Ibenge, ameamua kuvaa mabomu na kuwaambia ukweli mabosi, wapenzi na mashabiki wa timu hiyo, kwamba wawe watulivu na kila kitu kitakuwa sawa na ataitengeneza timu hiyo kufikia ubora ambao wanataka kuuona.

Azam inayoshiriki makundi ya CAF kwa mara ya kwanza kama ilivyo kwa Singida Black Stars, ipo Kundi B na ilianza na kichapo cha 2-0 kutoka kwa AS Maniema ya DR Congo kabla ya wikiendi iliyopita kulala tena 1-0 kwa Wydad Casablanca ya Morocco. Kundi hilo pia lina Nirobi United ya Kenya itakayocheza mechi mbili mfululizo zijazo dhidi ya Azam mapema mwakani.

Ibenge Atoa Neno  La Matumaini Azam Fc

Akizungumzia mwenendo wa  timu hiyo baada ya  kuhudumu kwa takribani miezi mine sasa, Ibenge alisema Azam bado iko salama katika hatua za kukua kwao, ambapo licha ya kupoteza mechi mbili za awali, matokeo hayo yatawajenga wachezaji wa kikosi hicho.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Ibenge alisema Azam haiwezi kufikia malengo yake ya kuwa klabu kubwa Afrika kwa kutumia msimu mmoja, na kwamba wataendelea kupitia hatua sahihi za ukuaji bila presha wala kuangalia wanapoanguka.

“Hakuna asiyeumizwa na matokeo mabaya, lakini kama unazingatia malengo na nini mlifanya kwenye mechi hizi mbili, ukiwa na timu ambayo ndiyo kwanza inacheza hatua kubwa kama hii unafurahishwa na juhudi za wachezaji wako,” alisema Ibenge na kuongeza.

Ibenge Atoa Neno  La Matumaini Azam Fc

“Azam FC haiwezi kuingia makundi kwa mara ya kwanza na kuchukua ubingwa, tutapita njia kama hizi za ukuaji ili tufike kuwa wakubwa zaidi kwa ubora uwanjani.

“Unakumbuka mara ya kwanza tulikuwa na malengo ya kufika makundi, hili lilipita na sasa tunaangalia nini tutakipata hapa kwenye makundi, lakini hatutakuwa kama tulivyocheza hivi kwenye mechi zinazokuja au hata msimu ujao. Naamini wachezaji wangu wamejifunza.”

Azam imeingia kwenye rekodi nyingine ya kutoshinda mechi tatu mfululizo, baada ya kupoteza mbili kwenye mashindano ya CAF na juzi kuambulia suluhu kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Singida Black Stars na kesho kutwa Desemba 7 watakuwa na vita ya kuwaania alama tatu mbele ya Simba kwenye Mzizima Derby, uwanja wa Mkapa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.