Zamalek Yapigwa Marufuku Usajili Kwa Madirisha Matatu

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeiwekea klabu ya Zamalek ya Misri marufuku mpya ya usajili kwa madirisha matatu, kufuatia kutokamilishwa kwa masuala ya kifedha ambayo yamekuwa yakiiandama timu hiyo kwa muda mrefu. Adhabu hiyo imeibuka wakati klabu hiyo ikiendelea kupambana kurejesha utulivu ndani na nje ya uwanja.

Ingawa FIFA haikutaja sababu rasmi katika taarifa yake, vyanzo vya kuaminika vimeeleza kuwa suala hilo linahusishwa moja kwa moja na malipo ambayo Zamalek inadaiwa kumlipa aliyekuwa kiungo wake, Ferjani Sassi. Kiungo huyo wa kimataifa kutoka Tunisia aliwakilisha klabu hiyo kwa mafanikio, lakini kuondoka kwake kuliacha mzigo wa deni ambalo hadi sasa halijalipwa.

Zamalek Yapigwa Marufuku Usajili Kwa Madirisha Matatu

Marufuku hiyo inamaanisha kuwa Zamalek haitaruhusiwa kusajili wachezaji katika madirisha matatu mfululizo ya usajili, hadi pale itakapokamilisha migogoro sita inayoendelea dhidi ya klabu hiyo. Hii ni pigo kubwa kwa mabingwa hao wa zamani wa Afrika, hasa wakati wakijaribu kujijenga upya na kurejea kwenye ushindani wa juu.

Hali hiyo huenda ikaleta changamoto kubwa kwa benchi la ufundi, ambalo sasa litalazimika kutegemea kikosi kilichopo kwa muda mrefu zaidi, bila nafasi ya kuongeza nguvu mpya. Mashabiki wa klabu hiyo tayari wameeleza wasiwasi wao, wakihofia athari za muda mrefu kwenye matokeo ya timu na mipango ya baadaye.

Zamalek Yapigwa Marufuku Usajili Kwa Madirisha Matatu

Kwa sasa, macho yote yameelekezwa kwa uongozi wa Zamalek kuona namna watakavyoshughulikia malalamiko yaliyopo ili kuondoa adhabu hiyo. Hata hivyo, hadi hapo mambo yatakaporekebishwa rasmi, marufuku hii itabaki kuwa moja ya changamoto kubwa zaidi kuwahi kukumba klabu hiyo yenye historia ndefu barani Afrika.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.