Kocha wa Liverpool, Arne Slot, amethibitisha tarehe ambayo Mohamed Salah ataungana na timu ya taifa ya Misri kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Salah anatarajiwa kujiunga na Misri mwishoni mwa mwezi huu kuelekea AFCON, ambalo litafanyika kuanzia Disemba 21 hadi Januari 18 nchini Morocco.
Mashindano hayo yamesogezwa mbele ili kufanyika katika kipindi cha msongamano wa mechi za sikukuu, na Misri ilikuwa na matarajio ya kumpokea Salah mapema kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki kabla ya AFCON dhidi ya Nigeria tarehe 14 Disemba.
Hata hivyo, Slot amethibitisha kuwa Salah hataruhusiwa kujiunga na timu ya taifa hadi Disemba 15, ikimaanisha kuwa atakuwepo kwenye mchezo wa Liverpool dhidi ya Brighton mwezi huu. Kutokana na AFCON, Salah anaweza kukosa hadi mechi sita, ikiwemo michezo ya Ligi Kuu dhidi ya Tottenham, Wolves, Leeds, Fulham na Arsenal, pamoja na mchezo wa Liverpool wa raundi ya tatu ya FA Cup mwezi ujao.

Misri ni miongoni mwa timu zinazopigiwa chapuo kwenda mbali na kutafuta taji lao la nane la AFCON. Liverpool sio timu pekee ya Premier League itakayopoteza wachezaji kwa AFCON; mahasimu wao Manchester United na Everton pia watakosa nyota wao muhimu.
Hata hivyo, Arsenal na Chelsea wanaowania ubingwa hawatapoteza mchezaji yeyote kwa safari ya Morocco, jambo litakalowawezesha kocha Mikel Arteta na Enzo Maresca kutumia kikamilifu vikosi vyao katika wiki zijazo.
Kwa upande mwingine, Salah atatumai kurejea kwenye kikosi cha kwanza cha Liverpool katika mchezo wa katikati ya wiki dhidi ya Sunderland, baada ya kukaa benchi bila kutumika kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham Jumapili.
Bao za kipindi cha pili kutoka kwa Alexander Isak na Cody Gakpo zilirudisha Liverpool kwenye njia ya ushindi na kupunguza presha kwa Slot, ambaye alikuwa kwenye msururu wa vipigo tisa katika mechi 12 zilizopita.



