Osimhen na Spalletti Kuungana Tena Kwenye Ligi ya Mabingwa

Mikutano ijayo ya Ligi ya Mabingwa kati ya Juventus na Galatasaray itaashiria kurejea kwa pamoja kwa Luciano Spalletti na Victor Osimhen, waliotwaa ubingwa wa Serie A wakiwa Napoli msimu wa 2022–23.

Osimhen na Spalletti Kuungana Tena Kwenye Ligi ya Mabingwa

Juventus wamepangwa dhidi ya Galatasaray kwenye mchujo wa hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa siku ya jana, jambo lililoandaa mkutano kati ya kocha wa Bianconeri, Spalletti, na mshambuliaji wa vigogo hao wa Uturuki, Osimhen.

Chini ya miaka mitatu iliyopita, wawili hao walitwaa ubingwa wa kihistoria wa Serie A wakiwa Napoli ubingwa wa kwanza kwa Partenopei baada ya miaka 33.

Osimhen alichangia kwa kiwango kikubwa mafanikio hayo kwa kufunga mabao 26, yaliyomfanya kuwa Capocannoniere (mfungaji bora) wa Serie A msimu wa 2022–23.

Kwa ujumla, Osimhen alifunga mabao 49 na kutoa pasi za mabao 12 katika mechi 71 chini ya Spalletti kwenye Uwanja wa Stadio Maradona.

Mshambuliaji huyo wa Nigeria alifunga mara tano katika michezo sita ya Ligi ya Mabingwa akiwa Napoli chini ya kocha huyo Muitalia, pamoja na mabao manne kwenye Ligi ya Europa msimu wa 2021–22, na mabao 40 katika misimu miwili ya Serie A.

Osimhen na Spalletti Kuungana Tena Kwenye Ligi ya Mabingwa

Spalletti aliacha Napoli mara baada ya kutwaa Scudetto mwaka 2023, huku Osimhen akikaa msimu mmoja zaidi kwenye Stadio Maradona kabla ya kujiunga na Galatasaray awali kwa mkopo mwaka 2024, kisha kusajiliwa moja kwa moja mwaka 2025.

Osimhen amefunga mabao 50 katika mechi 60 akiwa na vigogo hao wa Uturuki. Je nani kusonga mbele hatua inayofauta ya ligi ya Mabingwa?. Meridianbet inakwambia kuwa endelea kubashiri hapa kwani ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Ingia kwenye akaunti yako na uanze safari yako ya ushindi sasa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.