Simba Yakusanya Pointi 3 Kwa Mashujaa

Ligi kuu ya NBC Tanzania iliendelea hapo jana kwa mechi kadhaa ambapo mchezo wa mapema ulikuwa ni huu wa Simba dhidi ya Mashujaa na Mnyama aliibuka na magoli 2-0. 

Simba Yakusanya Pointi 3 Kwa Mashujaa

Goli la kwanza lilifungwa na Libase Gueye, huku ikiwa ndio mechi yake yakwanza kuichezea Simba huku akionyesha kiwango kilicholeta matumaini mapya ndani ya kikosi hicho katika ushindi wa mabao 2-0.

Goli la pili la kuipa Simba ushindi lilifungwa na Selemani Mwalimu na kuwafanya wasogee hadi nafasi ya 4 baada ya kuusanya pointi 16 kwenye ligi hadi sasa, huku Mashujaa wao wakibaki nafasi ya 8 na pointi zao 13.

Mchezaji huyo alitambulishwa mitaa ya Msimbazi Januari 17, 2026 akitokea Teungueth FC ya kwao Senegal, alifunga bao hilo dakika ya 27 kwa ufundi mwingi akimtesa kipa wa Mashujaa, Patrick Munthali.

Meridianbet inakwambia kuwa endelea kubashiri hapa kwani ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Ingia kwenye akaunti yako na uanze safari yako ya ushindi sasa.

Uchezaji wake wa kuhama upande kushoto na kulia, ulikuwa ukiwatesa walinzi wa Mashujaa wakiongozwa na nahodha, Mpoki Mwakinyuke, kuonyesha kuwa ubora wake ulionekana mwisho wa mchezo alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

Simba Yakusanya Pointi 3 Kwa Mashujaa

Dakika ya 40, Samson Madeleke katika jitihada za kumzuia Gueye, alijikuta akimchezea vibaya ndani ya boksi, mwamuzi Ahmed Arajiga kutoka Manyara akaamuru mkwaju wa penalti ambao hata hivyo, Kibu Denis aliyechukua jukumu la kupiga, akakosa baada ya Munthali kuokoa.

Hata hivyo, kipindi cha pili, mabadiliko yaliyofanywa kwa kuingia Seleman Mwalimu kuchukua nafasi ya Kibu, yalizaa matunda baada ya mshambuliaji huyo kufunga bao dakika ya 75.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.