Seleman Matola kocha msaidizi wa Simba SC amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara ya NBC dhidi ya Fountain Gate unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa jioni ya leo
Huu unakuwa mchezo wa kwanza kwa wekundu hao wa msimbazi msimu wa 2025/26 kwenye ligi ambayo imeanza kasi Septemba 17 kwa mechi za ushindani kuendelea ndani ya uwanja.
Simba SC imetoka kucheza mchezo wa kimataifa dhidi ya Gaborone United ya Botswana inakutana na Fountain Gate ambayo imetoka kupoteza mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Mbeya City kwa kufungwa bao 1-0.
Miongoni mwa wachezaji waliopo katika kikosi cha mnyama ni Ellie Mpanzu, Kibu Dennis, Moussa Camara, Ladack Chasambi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Kiujumla timu hizi mbili zimekutana mara tatu katika miaka ya karibuni huku Simba ikishinda mechi 2 na mmoja ukiisha kwa sare.
Matola amesema: “Tupo tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Fountain Gate ambacho tunahitaji ni matokeo na tunajua kwamba mchezo utakuwa na ushindani mkubwa tupo tayari na wachezaji wapo tayari mashabiki wajitokeze kwa wingi.”