Mikel Arteta, ameonyesha imani kubwa kwa Eberechi Eze baada ya kiungo huyo kufunga bao lake la kwanza kwa klabu hiyo katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Port Vale kwenye Kombe la Carabao, Jumatano usiku.
Eze alitikisa nyavu dakika ya nane tu katika uwanja wa Vale Park, akionyesha makali yake mapema. Hata hivyo, Arsenal walihangaika kutengeneza nafasi safi dhidi ya wenyeji wao wa Ligi ya Daraja la Kwanza, hadi Leandro Trossard alipoingia na kufunga bao la pili dakika ya 86, kuhitimisha ushindi.

Bao hilo lilikuwa la kwanza kwa Eze tangu atue Arsenal kwa dau la pauni milioni 60 kutoka Crystal Palace, na usiku huo alionekana kuwa mchezaji hatari zaidi katika safu ya ushambuliaji ya The Gunners.
Arteta alisema “Alicheza katikati dhidi ya timu iliyojipanga 5-4-1, wakibanana sana. Si rahisi kupata nafasi, lakini Eze ana uwezo mkubwa. Alifunga na pia alifanya matukio mengine matatu au manne ya hatari.”
Kocha huyo aliongeza kuwa Eze bado anahitaji muda zaidi kucheza na wachezaji wenzake ili kuelewa muda na mizunguko ya pasi, akisisitiza kuwa matukio kama hayo yatakuwa ya kawaida na yenye tija zaidi kwa timu.
Katika mechi hiyo, Eze alianza kushambulia kutoka upande wa kushoto, lakini tayari ameshachezeshwa katika nafasi mbalimbali na Arteta katika mechi tano alizocheza hadi sasa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.


