Kocha maarufu duniani, Jose Mourinho, ametangazwa rasmi kuwa meneja mpya klabu ya Benfica ya Ureno, akirejea katika klabu aliyowahi kuinoa miaka 25 iliyopita. Mourinho, mwenye umri wa miaka 62, amesaini mkataba wa miaka miwili, hatua inayofungua ukurasa mpya katika safari yake ya ukocha iliyojaa mafanikio makubwa.

Mourinho alianza safari yake ya ukocha Benfica mwaka 2000, lakini muda wake ulikuwa mfupi kabla ya kuhamia Uniao de Leiria mwaka uliofuata. Hapo ndipo nyota yake ilianza kung’aa, na mwaka 2002 alijiunga na FC Porto, ambako alijijengea jina kubwa kwa kutwaa mataji makubwa, ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Umaarufu pamoja na mafanikio yake ya nyuma yalimfikisha Chelsea mwaka 2004, kisha Inter Milan mwaka 2008, ambako alishinda treble ya kihistoria. Mwaka 2010 alihamia Real Madrid, akiongoza klabu hiyo kwa mafanikio makubwa. Alirudi Chelsea mwaka 2013 kwa awamu ya pili, kabla ya kuhamia Manchester United mwaka 2016, Tottenham Hotspur mwaka 2019, AS Roma mwaka 2021, na Fenerbahçe mwaka 2024.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.


