Kwa mara ya kwanza katika historia ya Klabu ya Dodoma Jiji FC imefanikuwa kuweka rekodi ya kutofungwa na Simba na kupata alama moja kwenye mgongo wa Simba. Mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya wenyeji, Dodoma Jiji dhidi ya Simba, ilimalizika kwa suluhu kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Mechi hiyo iliyokuwa na kasi kubwa huku ikitawaliwa na ushindani wa hali ya juu, ilishuhudiwa Simba ikitengeneza nafasi nyingi za kufunga, japo uimara wa kujilinda wa kikosi cha Dodoma Jiji βWalima Zabibuβ uliinyima kuondoka na pointi tatu.




