Ligi ya mabingwa Barani Afrika mechi za kukamilisha makundi na kutafuta timu 8 za kucheza robo fainali ilipigwa jana ambapo licha ya Yanga kushinda waliweza kutupwa nje ya michuano hiyo.

Vijana hao wa Pedro walishinda kwa mabao 3-0 wakiwa nyumbani, lakini ushindi huo si pekee ambao walikuwa wakiuhitaji bali pia walitarajia Al Ahly washinde ili wao wafuzu.
Ahly wakiwa kama vinara wa Kundi hilo B, walimaliza mechi kwa kutoa suluhu yaani 0-0 huku nafasi ya pili ikishikwa na ASFAR Rabat na 3 ikishikwa na Yanga wakati kwa upande wa Kabylie yeye akishika mkia.
Wananchi wamemaliza Kundi wakiwa na pointi 8 kwenye msimamo wa ligi huku Msemaji wa Klabu hiyo Ally Kamwe akisema kuwa wanajipanga kwaajili ya msimu ujao sasa wanwaekeza nguvu zao kwenye ligi.


