Ahmed Ally Ajimaliza, Loemba Ni Mtu Wa Kazi Sana

Meneja Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Ahmed Ally, ameonya wapinzani wa Ligi Kuu Tanzania Bara kuhusu ubora wa safu ya kiungo wa timu hiyo, akisema kuwa itakuwa changamoto kubwa msimu huu.

Kauli hiyo inakuja baada ya kiungo mshambuliaji, Iñno Jospin Loemba, kuonyesha kiwango cha juu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Petro de Luanda ya Angola.

Ahmed Ally Ajimaliza, Loemba Ni Mtu Wa Kazi Sana

Ahmed amesema  Loemba, ambaye alijiunga na Simba katika dirisha dogo la usajili, ameanza kuonyesha umuhimu wake katika timu kwa kuungana vyema na Clatous Chama.

“Loemba anacheza kama namba 8 au 10, lakini ana uwezo mkubwa, mawinga wanapaswa kujua jinsi ya kumtumia vyema,” amesema Ahmed.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Petro de Luanda, Loemba alionyesha kiwango bora licha ya kuingia akitokea benchi, akitoa pasi ya bao la kusawazisha lililofungwa na Anicet Oura.

Hii ilikuwa mechi yake ya kwanza tangu kujiunga na Simba, lakini alionyesha ufanisi mkubwa, na Ahmed alisisitiza kuwa uhusiano wake mzuri na Chama utakuwa na athari kubwa kwenye ligi.

Ahmed Ally Ajimaliza, Loemba Ni Mtu Wa Kazi Sana

“Ikiwa Loemba atapata uelewano mzuri zaidi na Chama, basi wapinzani wa Ligi Kuu Tanzania Bara watapata changamoto kubwa. Akielewana vizuri na Chama, watasema kwa lugha yao.” amesema na kuongeza kuwa;

Hii ni onyo kwa wapinzani wa Simba kwamba, pamoja na hali ya ushindani, safu ya kiungo ya timu hiyo itakuwa ni silaha muhimu katika mapambano ya ligi kuu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.