Yanga Matumaini Kibao Kwenda Robo Fainali

Uongozi wa klabu ya Yanga umeweka wazi msimamo wao wa kutokubali kushindwa, wakisema hawataki kutokea kile kilichotokea kwa wapinzani wao Simba,  walishindwa kufuzu kwa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa AS FAR Rabat kwenye mchezo wa ugenini uliochezwa dimbani Olymique, mjini Rabat, nchini Morocco.

Yanga Matumaini Kibao Kwenda Robo Fainali

Kipigo hiki kimewachia changamoto kubwa ya kupambana kwenye mechi yao ya mwisho ya makundi dhidi ya JS Kabylie ili kuepuka hatma ya kushindwa kufuzu kama ilivyotokea kwa Simba.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe, amesema kwamba kwa sasa klabu inawaona mbele tu, huku wakijua kwamba matokeo ya mchezo dhidi ya AS FAR Rabat hayawezi kubadilisha hali yao. Kamwe alisisitiza kuwa,

“Yanga kwa sasa tunawaza kushinda mechi yetu ya mwisho visiwani Zanzibar. Sio kushinda pekee, bali tunataka kufuzu kwenda robo fainali kwa ushindi mkubwa.”

Yanga Matumaini Kibao Kwenda Robo Fainali

Kamwe ameongeza kuwa wanajivunia uwezo wao na wana imani kwamba hakuna kitu kitakachowazuia kufuzu, “Tunataka kuonyesha maajabu kwa kushinda kwa kishindo na kufanya yote ili tufikie robo fainali.”

Wananchi wanahitaji ushindi katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya JS Kabylie utakaochezwa Jumapili, Februari 15, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Lakini si ushindi pekee, wanahitaji pia Far Rabat kupoteza mbele ya Al Ahly ili iweze kupata nafasi ya kusonga mbele. Katika kundi hili, Al Ahly anachukua nafasi ya juu akiwa na pointi tisa, AS FAR Rabat ina pointi nane na inashika nafasi ya pili, huku Yanga ikiwa na pointi tano.

Yanga Matumaini Kibao Kwenda Robo Fainali

JS Kabylie inashikilia mkia ikiwa na pointi tatu. Endapo Yanga itashinda mechi yake ya mwisho, huku Far Rabat akipoteza mbele ya Al Ahly, basi Yanga itafuzu kwa robo fainali.

Mechi hii itakuwa na umuhimu mkubwa kwa Yanga, kwani ushindi utahitaji jitihada za ziada na dhamira ya dhati, ili kuendelea kuandika historia yao katika michuano ya Afrika.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.