Kikosi cha Azam FC kimeondoka nchini alfajiri ya leo, Jumatano, kuelekea Casablanca, Morocco kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao muhimu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wydad AC. Huu ni mchezo ambao Azam FC wanaitaji matokeo ya ushindi pekee ili kupata nafasi ya kufuzu kuingia hatua ya robo fainali.

Msafara huo umejumuisha wachezaji kadhaa muhimu katika kila idara, huku makipa Aishi Manula, Zuberi Foba na Antony Mpemba wakiongoza safu ya walinda mlango.
Katika safu ya mabeki, Azam FC imewasafirisha Lusajo Mwaikenda, Pascal Msindo, Lameck Lawi, Twalib Nuru, Yoro Diaby, Nathaniel Chilambo, Ben Zitoune na Yeison Fuentes, wakitarajiwa kuwa nguzo imara katika kuzuia mashambulizi ya wenyeji wao.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa




