Ahmed Ally Awaunganisha Mashabiki Simba

Baada ya kuwa wanyonge sana msimu huu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba,  Ahmed Ally, amewataka wanachama kuungana na kuwa kitu kimoja katika kipindi na kuacha kutafuta nani mchawi wa matokeo mabovu kwa timu yao.

Ahmed alisema Wanasimba wanapaswa kuacha lawama na kulaumiana.  Badala yake waungane kwa pamoja na kuwapa sapoti wachezaji wao na timu yao kwa ujumla. Amesisitiza kuwa huu ni wakati wa mshikamano ili kukipa nguvu kikosi hicho katika mechi tatu zilizosalia za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Ahmed amesema bado ana imani kubwa kwamba Simba inaweza kufanya maajabu, kushinda mechi zote na kufuzu kwenda robo fainali endapo kila mmoja atatimiza wajibu wake.

Ahmed Ally Awaunganisha Mashabiki Simba

“Lawama hazijawahi kujenga mafanikio, bali huleta mpasuko ndani ya familia ya klabu. Kwa mujibu wake, huu ni muda wa kuimba wimbo mmoja na kusimama pamoja bila kujali changamoto zilizopita, kwani lengo kuu ni kuisukuma Simba mbele,” amesena na kuongeza;

Kuwa mechi ijayo dhidi ya Esperance ipo mikononi mwa Wanasimba wenyewe, na wakiamua kwa dhati, wapinzani wao watapata wakati mgumu Uwanja wa Benjamin Mkapa. Ahmed amesisitiza kuwa kipindi hiki Simba inawahitaji mashabiki wake zaidi kuliko wakati mwingine wowote, kila Mwanasimba kujitokeza kwa wingi uwanjani, akieleza kuwa ushindi wowote utakaopatikana ni wa klabu nzima.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Ameongeza kuwa Simba aliyoshuhudia Tunisia ilikuwa na kiwango kizuri,  anaamini kwa  Mkapa “utapasuka magoli”, kuwa kuwafunga wapinzani si kazi ya wachezaji pekee bali ni jukumu la mashabiki pia.

Amekumbusha historia ya Simba kama mmoja wa waanzilishi wa mashindano hayo Tanzania na klabu iliyozowea kufika robo fainali mara kwa mara. Ahmed amesema  kushindwa si lawama ya mtu mmoja, bali ni jukumu la wote, hivyo hakuna sababu ya kukubali kushindwa wakati uwezo upo, Simba haina budi kuingia kishujaa na kuipambania Esperance kwa umoja na ujasiri.

Ahmed Ally Awaunganisha Mashabiki Simba

Katika kuimarisha matumaini, Ahmed Ally amebainisha kuwa Simba inaendelea kujipanga vizuri zaidi, ikiwa ni pamoja na kuimarisha kikosi chake. Amesema Simba iliyoonekana Tunisia ilikuwa na mabadiliko makubwa na ilikosea mara moja tu, huku akiahidi kuwa Jumapili mashabiki wataiona Simba iliyokamilika zaidi. Pia ametangaza kuwa klabu iko tayari kumtambulisha mchezaji mpya aliyesajiliwa kupitia JayRutty, ambaye tayari amewasili nchini na taratibu zote zimekamilika.

Ahmed  amewataka Wanasimba wote kuipa nguvu  timu yao bila kukata tamaa, kuwa pointi tisa bado zipo mbele yao na robo fainali bado ipo mikononi mwa Simba. Amesema Simba kufanya maajabu inawezekana, ilimradi kila Mwanasimba asimame, aunge mkono timu na ajitokeze kwa wingi Uwanja wa Mkapa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.