Ligi kuu ya Hispania iliendelea kwa michezo kadhaa ambapo mechi kali kabisa ilikuwa hii ya El Clasico kati ya Real Madrid vs FC Barcelona ambapo mchezo huo ulimalizika kwa vijana wa Hans Flick kupigika kwa mabao 2-1.

Mabao hayo ya kuendelee kuiweka Real Kileleni yalifungwa na Kylian Mbappe na Jude Bellingham huku kwa upande wa Barca yakifungwa na Lopez. Vijana hao wa Xabi Alonso sasa wanakuwa mbele kwa pointi 5 huku mechi hiyo ikiwa ni ya kukata na shoka kabisa kwani kila mmoja alikuwa anahitaji ushindi.
Real Madrid wameweza kulipa kisasi cha kwanza wakiwa pale Santiago Bernabeu dhidi ya Barcelona ambao hawakupewa nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi kutoka na kuwepo na wachezaji wengi wenye majeraha akiwemo Raphinha, Lewandowski, na wengine wengi na hiyo ndio huenda ilifanya wapoteze.
Baada ya ushindi huo, Madrid atakuwa nyumbani tena kusaka pointi 3 dhidi ya Valencia, huku Barcelona wao pia watakuwa nyumbani kucheza dhidi ya Elche ambao wapo nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ligi. Je nani kuondoka na ushindi kwenye mechi hiyo?



