TRA United SC Yatua Rasmi Dar es Salaam

Klabu ya Tabora United, iliyokuwa ikiwakilisha mkoa wa Tabora katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, sasa imeingia katika sura mpya baada ya kununuliwa rasmi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kwa mabadiliko haya, jina la klabu limebadilishwa na sasa itajulikana kama TRA United SC.

Hatua hii pia imeambatana na uhamisho wa makazi ya klabu hiyo kutoka Tabora hadi jijini Dar es Salaam, jambo linaloifanya Dar es Salaam kuwa na jumla ya timu sita zinazoshiriki Ligi Kuu. TRA United SC inaungana na vigogo Simba SC, Yanga SC, Azam FC, KMC FC na JKT Tanzania katika kuwakilisha jiji hilo kwenye medani ya soka la ushindani.

TRA United SC Yatua Rasmi Dar es Salaam

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Mabadiliko haya yanachukuliwa kama sehemu ya juhudi za kuimarisha miundombinu na usimamizi wa klabu, huku TRA ikilenga kuleta mapinduzi ya kiutawala na kiufundi ndani ya timu. Mashabiki wa soka wanatazamia kuona kama uhamisho huu utaleta mafanikio mapya kwa klabu hiyo iliyokuwa na mizizi ya muda mrefu mkoani Tabora.

Kwa sasa, Dar es Salaam inazidi kujikita kama kitovu cha soka nchini Tanzania, na ujio wa TRA United SC unazidisha ushindani na msisimko katika Ligi Kuu. Je, klabu hii mpya itaweza kujenga historia mpya jijini, au itakumbwa na changamoto za kuzoea mazingira mapya?

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.