Walter Harrison Ampa Maua Yake Diarra

Meneja wa Klabu ya Yanga Walter Harrison amemmwagia sifa kipa namba moja wa timu hiyo raia wa Mali Djigui Diarra kuwa ni mtu wa maana ambaye hapendi kupoteza wala kuruhusu bao kwenye mechi hata kama atakuwa amefungwa.

Walter alisema, Diarra ni kiungo muhimu kwenye timu hiyo na ni kati ya   wachezaji viongozi kwenye timu na anapenda kushinda na timu yake kupata mafanikio makubwa kwenye timu na huwa anakosa amani kila mara timu inapopitia magumu au kupoteza mchezo.

Walter Harrison Ampa Maua Yake Diarra

“Niwe mkweli kabisa, Diarra ni mtu ambaye anaipenda sana kazi yake na kama unaangalia michezo utagundua kuwa hapendi kufungwa kabisa, hilo ni kosa.

“Yaani hata kama tufunge goli 5 ila yeye kuruhusu bao moja tu ni dhambi kubwa sana na anakuwa anagombana sana na wachezaji wenzake pindi inapotokea hali kama hiyo kwa hiyo kwenye kazi yake, amenyooka.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

“Nje ya uwanja ni mtu anayejipenda na anapenda sana mazingira ya Tanzania unaweza ukafikiri kama ni mwenyeji yaani kashakuwa mtanzania. 

“Ni mtu fulani ambaye mtulivu sana, anakaa sana nyumbani lakini pia anaangalia jinsi ya kusaidia watu wengine ambao wanamzunguka ili kuweza kutimiza ndoto zao.

Walter Harrison Ampa Maua Yake Diarra

“Mimi nina stori moja ya mtu mmoja, sitomtaja jina lakini ni mchezaji mkubwa na alipata changamoto. Tukiwa Algeria nilikuwa nawasiliana naye na kuniambia ana changamoto nyingi zimetokea na ni changamoto zilizomfanya ashuke sana kiuchumi. 

“Amepata majeraha makubwa yaliyomfanya atumie hela nyingi takribani dola 20,000 kufanya operesheni. Akanambia kuwa Diarra amekuwa kama mzazi kwake kwani anamsaidia chakula na kila anachohitaji.” Alisema Walter.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.