Klabu ya Liverpool chini ya kocha mkuu Arne Slot imezidi kupata mwendelezo mbaya wa matokeo kwenye ligi kuu baada ya kupoteza mechi yake ya 4 mfululizo wikendi hii dhidi ya Brentford.

Liverpool kabla ya mchezo huo wa Jumamosi ambao ulipigwa huko Gtech Community walikuwa wamepata ushindi mnono kabisa kwenye ligi ya mabingwa ambao ulifanya watu wengi waamini kuwa Jogoo huyo wa Anfield amerejea kwenye kiwango chake, kabla ya dakika 90 kukamilika kwa kupoteza mechi.
Ni Brentford ndio ambao walianza kupachika mabao kupitia kwa mchezaji wao Outtara ambapo Kerkez alikuja kuifungia Liver goli la kwanza baada ya Schade kufunga bao la pili huku wakienda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao 1.
Kocha mkuu wa Liverpool licha ya kufanya mabadiliko ya wachezaji lakini bado walishindwa kuondoka na ushindi ugenini na kufanya kuwa mechi ya nne mfululizo bila ya ushindi kwenye EPL na hivyo kushuka hadi nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi, wakati Nyuki wao wakipanda nafasi ya 11.



