Pale ambapo wengi walidhani Manchester City wameondoka kabisa katika kinyang’anyiro cha ubingwa Ligi Kuu ya Uingereza, Bernardo Silva na Erling Haaland wamejitokeza wakiwaacha Liverpool wakiwa na mshangao na Arsenal wakitazama kwa hofu.

Anfield imekuwa ngome isiyopinduliwa kwa Liverpool, lakini mechi ya Jana ilionyesha kitu kisichowahi kushuhudiwa, matokeo ambayo hayajaonekana tangu mwaka 2003.
Ushindi wa mwisho wa City Anfield mbele ya mashabiki ulikuwa mwaka 2003, wakati Kevin Keegan akiwa meneja, Maine Road ikiwa uwanja wao, na Peter Schmeichel akiwa mlinda mlango. Pep Guardiola amekuwa akikosa kabisa matokeo Anfield, lakini hapo jana, kocha huyo Muhispania aliandika kumbukumbu mpya kama kocha wa Manchester City.
Nusu ya kwanza ilionekana kuwa ni ya City, wakidhibiti mpira na kushambulia kwa ufanisi. Lakini Liverpool walijitokeza, na Dominik Szoboszlai aliweka kimyani kwa shuti la faulu na kuipa Liverpool bao la kuongoza, wakiwacha City nyuma.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa


