Kwa mujibu wa Tuttosport, Manchester United watapeleka maskauti kuwafuatilia Federico Dimarco wa Inter na Pierre Kalulu wa Juventus katika mechi ya Derby d’Italia itakayochezwa Jumamosi.

Gazeti la Tuttosport linaripoti kuwa Mashetani Wekundu watafuatilia kwa karibu Derby d’Italia ya kesho kati ya Inter na Juventus. Gazeti hilo la mjini Turin linadai kuwa Manchester United wameelekeza macho yao kwa Dimarco na Kalulu.
Kalulu amekuwa chaguo la kwanza katika kikosi cha Juventus msimu huu, akicheza chini ya Igor Tudor na Luciano Spalletti. Katika sehemu ya kwanza ya msimu alicheza kama beki wa pembeni wa kulia (right wing-back), na chini ya kocha mpya wa Juventus amecheza kama beki wa kati na beki wa kulia katika mfumo wa mabeki wanne.
Ana mkataba wa muda mrefu katika Uwanja wa Allianz hadi Juni 2029, huku mkataba wa Dimarco na Inter ukiwa unasalia na takribani miezi 18 kabla ya kumalizika.
Kwa mujibu wa Tuttosport, beki huyo wa kushoto wa Italia alikuwa tayari kusaini mkataba mpya mwaka jana, na sasa Nerazzurri wako tayari kuwasilisha ofa ya mkataba mpya hadi mwaka 2030.


