Kocha Mkuu wa Singida Black Stars, David Ouma, amesema kikosi chake kinaelekea Afrika Kusini kikiwa na lengo la kulinda heshima katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch FC. Mchezo huo utapigwa Jumapili kuanzia saa 1:00 usiku, huku timu zote zikiwa tayari zimepoteza nafasi ya kufuzu hatua inayofuata.
Ouma amesema ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fountain Gate kwenye ligi ya ndani umeongeza morali ya wachezaji, na kwa sasa hakuna majeruhi kikosini. Ameeleza kuwa licha ya kutokuwa na nafasi ya kusonga mbele, timu hiyo itaingia uwanjani kwa nidhamu, ushindani na heshima kwa mashindano hayo ya kimataifa.
“Hatuna cha kupoteza. Kufika hapa tayari ni hatua kubwa kwetu kwa sababu ni mara yetu ya kwanza kushiriki mashindano haya. Tumejifunza mengi, ikiwemo namna ya kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani,” amesema Ouma, akisisitiza kuwa uzoefu walioupata utakuwa msingi wa mafanikio yajayo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa




