Singida Wanataka Kutamba Pande Za Wakongo

Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS Otoho umeanza  kumpa nguvu ya kujiamini Kocha wa Singida Black Stars, David Ouma ambaye amesema wanaenda kuandika historia nyingine kumataifa kwa kupata pointi tatu wakiwa ugenini.

Wachezaji 21 wa Singida Black Stars, wapo  nchini Congo kucheza mechi ya nne hatua ya makundi katika Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Otoho d’Oyo itakayofanyika Februari 1, 2026.

Singida Wanataka Kutamba Pande Za Wakongo

Mchezo ambao kama wakishinda utawaongezea matumaini zaidi ya kuvuka hatua ya makundi na kwenda hatua ya mtoano kwa maana ya robo fainali ambayo itakuwa ni kwa mara ya kwanza katika historia yao wanacheza hatua hiyo.

Ouma ambaye ni raia wa Kenya amesema wanaenda kucheza mchezo mgumu ambao wao wameubeba kama fainali kwani umeshikilia uamuzi wa nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali ambayo ameitaja kuwa itabaki katika historia bora kwa klabu yao.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Singida Wanataka Kutamba Pande Za Wakongo

“Tunakwenda tukiwa na malengo sawa kuanzia benchi la ufundi hadi wachezaji, hivyo mipango ipo vizuri na kila mchezaji anatambua umuhimu wa mchezo huo ambao kwetu ni kama fainali kutokana na kubeba hatma yetu. 

“Hatutarajii mchezo rahisi, tumejiandaa kwenda kushindana na kucheza kwa kumuheshimu mpinzani wetu ambaye pia anasaka pointi tatu kama ilivyo upande wetu, mbinu bora na kujitoa kwa wachezaji ndio kutatupa nafasi ya kusonga nafasi inayofuata,”  amesema Ouma.

Ouma amesema anatambua ubora na upungufu wa wapinzani wao, hivyo amefanyia kazi katika uwanja wa mazoezi na ataendelea kusuka mbinu bora kabla ya mechi hiyo.

Singida Wanataka Kutamba Pande Za Wakongo

Wachezaji wa Singida Black Stars walioondoka ni Metacha Mnata, Amas Obasogie, Abdallah Said ‘Lanso’, Miraj Hassan, Kennedy Juma, Mukrim Issa, Abdulmalick Zakaria, Idd Khalid, Morice Chukwu na Khalid Aucho.Wengine ni Emmanuel Keyekeh, Idriss Diomande, Marouf Tchakei, Mtange Linda, Deus Kaseke, Lamine Jarjou, Mossi Nduwumwe, Joseph Guede, Harson Muaku, Mishamo Daudi na Elvis Rupia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.