Yanga Kuwafanyia Umafia JS Kabylie Mechi ya Mwisho

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, amesema kikosi hicho kitaingia na sura mpya ya kiuchezaji kitakapomenyana na JS Kabylie katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Jumapili, Februari 15, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Yanga Kuwafanyia Umafia JS Kabylie Mechi ya Mwisho

Kamwe amesema kocha mkuu Pedro Goncalves ameandaa mbinu tofauti kwa ajili ya mchezo huo muhimu, akisisitiza kuwa mashabiki watashuhudia mabadiliko ya kimkakati ambayo hayajaonekana katika mechi zilizopita za michuano hiyo. “Wapo waliokuwa wakisema kocha wetu anacheza kwa tahadhari. Mechi ya Jumapili wataiona sura yake nyingine kabisa,” amesema Kamwe.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Yanga Kuwafanyia Umafia JS Kabylie Mechi ya Mwisho

Yanga inaingia katika pambano hilo ikiwa inahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya robo fainali. Katika kundi hilo, vinara ni Al Ahly SC wenye pointi tisa, wakifuatiwa na AS FAR Rabat wenye pointi nane. Yanga ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama tano huku JS Kabylie wakishika mkia kwa pointi tatu.

Kwa mujibu wa Kamwe, Yanga tayari imepata uzoefu wa kutosha katika kundi hilo baada ya kukutana na wapinzani wote, jambo linalowapa imani ya kumaliza hatua ya makundi kwa nguvu. Ameeleza kuwa lengo la klabu hiyo ni kufuzu kwa kishindo na kuingia robo fainali wakiwa na morali ya juu.

Yanga Kuwafanyia Umafia JS Kabylie Mechi ya Mwisho

Katika kuhakikisha sapoti inakuwa ya kutosha, Kamwe amesema mashabiki wengi wa Yanga wamejipanga kusafiri hadi Zanzibar kuishangilia timu yao. Aidha, mfadhili wa klabu hiyo, Said Ghalib (GSM), anatarajiwa kuwepo uwanjani kushuhudia timu hiyo ikisaka ushindi muhimu katika pambano hilo la maamuzi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.