Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara inaendeea hii leo kwa mchezo mmoja ambapo klabu ya Simba watakuwa ugenini kumenyana dhidi ya Ihefu majira ya saa 10:00 jioni katika dimba la Highland Estate Mbarali.

Simba na Ihefu wametoka kukutana kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam ambapo vijana wa Mbeya walipoteza kwa mabao 5-1 huku Jean baleke akiondoka na Hat-trick.
Kwenye msimamo wa ligi kuu Simba yupo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi zake 24 akiwa ameshinda mechi 17, sare 6 na kupoteza mara 1 huku akijikusantia pointi 57 hadi sasa.

Ihefu yeye yupo nafasi ya 7 akiwa kacheza mechi zake 25 na pointi 33, ushindi ni mechi 10, sare 3 na kupoteza mara 12. Vile vile ametoka kushinda mechi mbili mfululizo kwenye ligi kuu.
Ikumbukwe kuwa mpaka sasa ni Ihefu pekee ambayo amemfunga kinara wa ligi Yanga akiwa nyumbani kwake lakini hakuishia hapo amemfunga na Azam pia. Je leo hii anaweza kufanya hivyo hivyo kwa mnyama?

