TFF Yafungia Uwanja wa KMC Complex

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuufungia Uwanja wa KMC Complex, uliopo Mwenge, Dar es Salaam kutumika kwa michezo ya Ligi Kuu, kutokana na kukosa vigezo vinavyohitajika.

TFF Yafungia Uwanja wa KMC Complex

Taarifa hiyo  imetolewa leo Alhamisi, Januari 29, 2026, na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Ndimbo, TFF imesema uwanja huo haujakidhi matakwa ya Kanuni kama yalivyoainishwa kwenye masharti ya Leseni za Klabu, hali iliyolazimu kuchukuliwa kwa uamuzi huo.

Shirikisho hilo la Soka limeeleza kuwa, kuanzia sasa, timu zote zinazoutumia Uwanja wa KMC kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutumia viwanja mbadala, kama kanuni zinavyoelekeza, hadi pale uwanja huo utakapofanyiwa marekebisho.

“Timu husika zitatumia viwanja vingine kwa michezo yao ya nyumbani mpaka Uwanja wa KMC utakapofanyiwa marekebisho na kukaguliwa upya na TFF,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Shirikisho hilo pia limetumia fursa hiyo kuzikumbusha klabu zote nchini kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja vyao ili kukidhi vigezo vya mashindano.

TFF Yafungia Uwanja wa KMC Complex

KMC hadi sasa kwenye ligi kuu imekuwa na mwenendo mbaya wa matokeo, anashika mkia na pointi zake 5 kwenye michezo 11 ambayo amecheza hadi sasa.

Je msimu huu wanaweza kumaliza nafasi ya ngapi?. Au wanaweza kushuka daraja na je mwalimu Bares anatakiwa kufanya nini kuhakikisha timu hiyo haishuki daraja?

 

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.