Yanga Bado Inawatesa Mashujaa Fc

Haijawa rahisi kwa Kocha Mkuu wa Mashujaa FC Salumu Mayanga, kuweza kusahau kipigo cha mabao 6-0 dhidi ya Yanga ugenini, baada ya kocha huyo, kufichua kwamba walifanya makosa ambayo bado yanamsumbua kuyatatua kabla ya kukutana na mpinzani mwingine ambaye ni Simba.

Mashujaa walijikuta wanapoteza kwa idadi hiyo ya mabao kwa mara ya kwanza msimu huu na kuwa timu ya kwanza kupigwa nyingi na Yanga tangu kuanza kwa mwaka huu wa mashindano ya ligi kuu. Mchezo ambao ulichezwa Januari 19, 2026, kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

Yanga Bado Inawatesa Mashujaa Fc

Hii imekuwa ni kama mazoea kwa Yanga kuishushia Mashujaa kipigo kikali kwani msimu uliopita iliichapa 5-0 nyumbani kwao KigomaAkizungumza na Soka la Bongo, Mayanga amesema waliingia kwenye mchezo huo na mipango mizuri ya kuwaheshimu wapinzani lakini bao la mapema dakika ya nane lilitibua kila kitu na kuwachanganya wachezaji.

“Matokeo hayo nimeyapokea, lakini yalilivuruga benchi na wachezaji kwa ujumla kwani ni kipigo kikubwa ambacho hatukukitarajia. Hatuwezi kurudia makosa haya kwani tayari nimeanza kufanyia kazi upungufu uliotugharimu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Ni kweli tulikutana na mpinzani bora, lakini hatukustahili matokeo haya kama tusingefanya makosa, naamini wachezaji wangu pia waliumizwa na matokeo yale, hivyo hawatakubali kurudia makosa kama waliyofanya kuelekea mechi zijazo,” amesema Mayanga.

Yanga Bado Inawatesa Mashujaa Fc

Mayanga amesema wamekutana na wananchi mara nyingi na kufanikiwa kudhibiti ubora wao lakini mchezo uliopita walizidiwa na kujikuta wakiruhusu mabao mengi. Amesema wametambua makosa na kuyafanyia kazi licha ya kwamba haikuwa rahisi kutokana na saikolojia ya wachezaji wake kutokuwa sawa.

“Haikuwa rahisi kusawazisha makosa kwani wachezaji pia hawakuwa katika hali nzuri kwani kipigo kilikuwa ni kikubwa, hawakukitarajia lakini kama benchi la ufundi tumefanya kazi ya ziada kuhakikisha tunawajenga wachezaji na wanarudi kwenye mstari wa ushindani,” amesema

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.