Yanga Yatoa Dozi Nzito Dhidi ya Mashujaa

Ligi kuu ya NBC Tanzania jana iliendelea kwa mchezo mmoja ambapo bingwa mtetezi Yanga alikuwa nyumbani kumenyana dhidi ya Mashujaa na akafanikiwa kushinda kwa mabao 6-0.

 

Yanga Yatoa Dozi Nzito Dhidi ya Mashujaa

Mchezo huo ambao ulipigwa majira ya saa 10:00 katika dimba la KMC Complex ulimalizika kwa Wanachi kukusanya pointi 3 na uhsindi wa kishindo huku mashabiki wakifurahi kabisa kuona ubora wa klabu yao.

Mpaka kufikia mapumziko Yanga walikuwa wanaongoza kwa 3-0, huku wakiukamata mchezo kwa asiliia kubwa kabisa na burudani ambayo ilitolewa ilikuwa ni ya hali ya juu.

Mabao hayo ya kuimaliza Mashujaa FC yalifungwa na Damaro, Abuya, Pacome, Dube, Mudathir, pamoja na Depu ambaye ni usajili mpya wa Wananchi.

Kwa ushindi huo sasa Yanga wapo nafasi ya kwanza wakiwa na pointi zao 19 baada ya michezo 7 ambayo wamecheza hadi sasa, huku kwa upande wa Mashujaa wao wamesalia nafasi ya 5 wakiwa na pointi zao 13 hadi sasa.

Yanga Yatoa Dozi Nzito Dhidi ya Mashujaa

Baada ya mchezo huo vijana wa Pedro watasafiri kukipiga dhidi ya Al Ahly kwenye Ligi ya mabingwa ambapo mpaka sasa wapo nafasi ya 2 wakiwa na pointi 4 kwenye msimamo wa Kundi lao.

Meridianbet inakwambia kuwa endelea kubashiri hapa kwani ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Ingia kwenye akaunti yako na uanze safari yako ya ushindi sasa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.