Al Ahly Waingia Kwenye Mtego Wa Yanga

Uongozi wa klabu ya Yanga umetuma ujumbe mzito kuelekea mchezo wao wa Jumamosi, Januari 31 dhidi ya Al Ahly, ameeleza wazi kuwa pambano hilo limebeba hatma ya timu hiyo kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa kutambua uzito wa mechi hiyo ya maamuzi, kikosi cha Yanga kimeondoka leo kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kambi maalum ya maandalizi ya mwisho kabla ya kuivaa Al Ahly mchezo wa marudiano utakaopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex.

Al Ahly Waingia Kwenye Mtego Wa Yanga

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema mechi ya Jumamosi ni karata ya mwisho kwao na haina nafasi ya makosa, akibainisha kuwa ushindi pekee ndio utakaowaweka hai kwenye mbio za kusonga mbele.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Kuifunga Al Ahly kunahitaji akili, nidhamu na utulivu mkubwa. Tumekuja Zanzibar tukiwa tumepanga kila kitu, hatutacheza na Al Ahly kichwa kichwa kwa sababu waarabu sio watu rahisi kabisa,” amesema Kamwe.

Al Ahly Waingia Kwenye Mtego Wa Yanga

Kamwe ameongeza kuwa Yanga inaufahamu vyema ubora wa Al Ahly pamoja na uzoefu wao mkubwa katika michuano ya Afrika. Ameweka wazi kuwa benchi la ufundi na wachezaji wake wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanapigania ushindi mbele ya mashabiki wao.

Kwa mujibu wa Kamwe, mchezo wa Jumamosi sio wa kawaida, bali ni vita ya heshima, historia na ndoto ya Yanga kuandika ukurasa mpya katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.