Masha Apewa Tuhuma Kuvujisha Siri za Sundowns

Klabu ya Mamelodi Sundowns FC imemchukulia hatua kali video analyst wake, Mario Masha, kwa kumsimamisha kazi kufuatia tuhuma za kusambaza taarifa za siri za benchi la ufundi linaloongozwa na Miguel Cardoso.

Kwa mujibu wa taarifa zinazoendelea kusambaa, Masha anatuhumiwa kuvujisha mbinu na mipango ya kiufundi ya timu hiyo kwenda kwa benchi la MC Alger jambo linalodaiwa kuhatarisha ushindani na maandalizi ya Sundowns katika michuano husika.

Masha Apewa Tuhuma Kuvujisha Siri za Sundowns

Hatua hiyo inakuja katika kipindi ambacho kumekuwa na mabadiliko kadhaa ndani ya klabu hiyo. Hivi karibuni, mchambuzi mkuu wa timu, Goolam Valodia, naye aliondoka baada ya kuitumikia Sundowns kwa takribani miaka 15.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Mario amekuwa sehemu ya familia ya Sundowns kwa zaidi ya muongo mmoja, akihudumu chini ya makocha mbalimbali waliopita katika klabu hiyo akiwemo Pitso Mosimane, Manqoba Mngqithi, Rhulani Mokwena na sasa Miguel Cardoso.

Masha Apewa Tuhuma Kuvujisha Siri za Sundowns

Mpaka sasa, klabu haijatoa taarifa rasmi ya kina kuhusu hatma ya mwisho ya Masha, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu ufafanuzi zaidi kuhusu sakata hilo linalotikisa moja ya vilabu vikubwa barani Afrika.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.