Wakati Fountain Gate na Namungo zikiwa viwanja tofauti kusaka pointi Ligi Kuu Bara, unaweza kusema hali ni tete kwa timu hizo ndani ya raundi tano zilizopita sawa na dakika 450 kwani zimeshindwa kuibuka na ushindi.

Katika mechi tano zilizopita, Yanga ndiyo iliyokusanya pointi nyingi zaidi ambazo ni 18 dhidi ya Namungo (1-0), Dodoma Jiji (3-1), Mashujaa (6-0), Coastal (1-0), Fountain Gate (2-0) na JKT (5-0).
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Fountain Gate na Namungo zimeambulia pointi mbili kati ya 15 kila mmoja akichapwa mechi tatu na sare mbili.Kipigo ambacho Namungo ilikumbana nacho dhidi ya Yanga Jumapili iliyopita kilikuwa cha tatu mfululizo baada ya kile cha Tanzania Prisons 3-2 na Pamba Jiji 1-0. Kabla ya hapo zilitoka sare mbili dhidi ya Mtibwa na Fountain Gate kwa bao 1-1 katika kila mechi.
Kwa upande wa Fountain ambayo ipo nafasi ya 15 kati ya timu 16 mara ya mwisho ilifungwa bao 1-0 na Singida Black Stars lakini kabla ya hapo sare mbili mfululizo dhidi ya Namungo 1-1 na Azam 0-0. Katika mechi mbili za kwanza ilipoteza dhidi ya Yanga na JKT Tanzania katika kila mechi 2-0.


