Dube Apewa Ujumbe Wa Matumaini Na Ali Kamwe

Watu wote watakuwa wanakubali kuwa mshambuliaji wa Yanga, raia wa Zimbabwe Prince Dube, anapitia kipindi kigumu sana ndani ya Yanga, baada ya kukaa muda mrefu bila kupata bao.

Mbaya zaidi, wakati timu yake ikiwa inapambana kwenda makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, alikosa nafasi ya wazi iliyokuwa inamaliza kabisa mchezo  kwa kuipa timu hiyo bao la tatu. Lakini ikashindikana na akaomba mwenyewe kutolewa.

Kufuatia hali hiyo, Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, ametoa ujumbe mzito wa kumtia nguvu mchezaji huyo kwenye kipindi hiki kigumu anachopitia.

Dube Apewa Ujumbe Wa Matumaini Na Ali Kamwe

Kamwe amesema: “Imani ni kwake Baba aliye juu Mbinguni, Prince.

“Kuna nyakati Mwanadamu unaweka sana jitihada kwenye Maisha, unavuja jasho lako lote, unatumia nguvu zako na uwezo wako wa kila aina, lakini mwisho wa siku haupati matokeo unayoyatamani.

“Inatokea hii Dube. Inaweza kumtokea Mkulima shambani, inaweza kumtokea Mama sokoni na inaweza kumtokea Ronaldo kwenye uwanja wa mpira.

“Inamtokea Yeyote. Kipindi unachopitia sasa hivi Dube uwanjani kinaweza kumtokea mwanadamu yeyote anayevuta pumzi ya Mungu duniani.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Dube Apewa Ujumbe Wa Matumaini Na Ali Kamwe

“Walio salama ni wale tu walio lala futi 6 chini ya tumbo la ardhi. Lakini kama bado uko hai, unapumua, tegemea jaribu la Mungu wakati wowote.

“Na sio kwamba hufanya hivyo kwa kuwa anatuchukia, hapana. Jaribu lolote lile, kubwa au dogo huja kwa ajili ya kutukumbusha kuwa, tuko sisi tunaotamani na yuko yeye muumba, anayepanga.

“Matamanio yetu ya mambo au vitu vizuri yanahitaji mpango wake. Ukikosa leo, unatakiwa usiku urudi tena kwenye sala, kumuomba akupangie kesho nzuri.

“Tunapaswa kumuomba na kumtegemea Mungu Pekee.  Wanaofeli duniani sio wale wanaokosa bali ni wale wanaopoteza imani. Najua Imani yako ni Imara sana.

Dube Apewa Ujumbe Wa Matumaini Na Ali Kamwe

“Jumbe zote za mashabiki wa Yanga ni za kukumbusha kuwa, wewe ni sehemu ya familia yetu. Tulishawahi kupita kwenye hali kama hii ya leo huko nyuma, Na tukasimama na wewe pamoja.

“Wananchi wanakuahidi kusimama na wewe Tena, kwa sala na maombi na In Shaa Allah. Furaha itarudi tena kwenye uso wako na kwenye mioyo yao tukiruka na kushangilia mabao yao uwanjani.

“Wanayanga wanaona jitihada zako. Wanaona unavyokimbia zaidi uwanjani kuipambania timu ishinde, kinachokosena ni magoli tu kutoka mguuni mwako. Tuna imani kubwa yatapatikana. Tunaomba na wewe uamini pia. Tuko pamoja.

Tuweke kichwa juu Prince Dube na In Shaa Allah, Mashabiki wa Yanga, watakuja tena KMC kukushangilia kwa sauti ya juu ukiwa kwenye Jezi yao,” alisema Ali.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.