Kuelekea mchezo wa CAF Champions League kati ya Yanga SC dhidi Silver Strikers FC unaotarajiwa kuchezwa jioni ya leo nchini Malawi, Yanga wameendelea kuimarika zaidi baada ya wachezaji wake Clement Mzinze na Mohamed Hussein Tshabalala kuanza matizi kwa maandalizi ya mwisho.
Mzize alikosekana kwenye kikosi cha Yanga kwenye mechi mbili za mwisho kwa sababu ya majeraha, kadhalika pia kwa Tshabalala ambaye alikuwa akichechemea kwa maumivu pia. Msafara wa Yanga SC uliojumuisha wachezaji 24 uliwasili salama Malawi, Oktoba 16 2025 na kuanza kufanya mazoezi chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz.
Mkuu wa msafara huo kwa wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Alex Ngai ambaye yupo na timu nchini Malawi. Na alisema kuwa kila kitu kinakwenda sawa kwa upande wa timu hiyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Kwa upande wa Afisa Habari wa timu hiyo Ali Kamwe alisema, hali ya mambo ipo sawasawa na wameshanza maandalizi haraka kuelekea kwenye mechi hiyo Ambayo ina umuhimu mkubwa kwao kushinda.
“Tunashukuru Mungu kuwa kila kitu kinaenda sawa, mapokezi ni mazuri kwa watu wa hapa Malawi na tayari mipango imeanza kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mchezo huu,” alisema Kamwe.
Haya ni maandalizi ya mwisho kwa Yanga SC kucheza mchezo wa ugenini kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.