Yanga Vitani Leo Caf Champions League Nchini Malawi

Wawakilishi wa Tanzania katika anga la Kimataifa Yanga, wanatarajia kutupa karata yao ya kwanza leo kwenye ardhi ya Malawi kusaka nafasi ya kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo Oktoba 18, 2025 Uwanja wa Bingu saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki.

Yanga walifanya shughuli mbalimbali za kijamii  nchini humo ikiwemo kuitembelea familia ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo miaka ya nyuma, marehemu Jacky Chamangwana.

Yanga Vitani Leo Caf Champions League Nchini Malawi

Baada ya mchezo huu wa leo kituo kinachofuata itakuwa ni Yanga kuwakaribisha Silver Strikers FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 25, 2025 na huu ni mchezo ambao utaamua mshindi atakeyetinga hatua ya makundi.

Aziz Andambwile kiungo wa Yanga SC amesema wapo vizuri kuwakabili Silver Strikers ya Malawi kwenye mchezo wa ugenini na benchi la ufundi limewapa maelekezo yakufanyia kazi.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Ikumbukwe kwamba kwenye mechi za awali Andambwile alifunga magoli mawili alianza ugenine na moja alifunga Uwanja wa Mkapa walipotinga hatua inayofuata kwa jumla ya magoli 5-0 Wiliete vijana wa Angola.

Yanga Vitani Leo Caf Champions League Nchini Malawi

Andambwile amesema: “Tunaamini mchezo utakuwa mgumu, wachezaji tumejiaanda vizuri kwa asilimia 90 tupo tayari ili kupata matokeo mazuri katika mchezo wetu.

“Kuna namna ambavyo tumepewa maelekezo kwa ajili ya mchezo wetu. Timu ambayo tunacheza nayo ni nzuri na tunaamini mchezo utakuwa mzuri nasi wachezaji tupo tayari,” amesema Andambwile.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.