Yanga Presha Kubwa Kuelekea Kufuzu Makundi

Inaelezwa viongozi wa Yanga wamekuwa na presha kubwa kuelekea kwenye mechi yao ya kesho dhidi ya Sliver Strikers wakiwa na uhakika mdogo wa kama watafuzu kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Yanga Presha Kubwa Kuelekea Kufuzu Makundi

Hiyo ni kutokana na kwamba wapo nyuma kwa bao 1-0, wakipoteza ugenini kule Malawi na jambo lingine, ni namna ambavyo Wamalawi hao walivyoingia kibabe nchini jana wakiwa na ujumbe wakuwaΒ  wanakwenda kufuzu.

Inadaiwa vikao ni vingi Jangwani vinavyofanywa na mabosi wa Yanga sambamba na wachezaji na benchi la ufundi la timu hiyo ili kuweka mambo sawa kuelekea mechi hiyo ya marudiano.

Yanga itakuwa mwenyeji wa Silver Strikers katika mechi ya marudiano kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo, itakayochezwa Jumamosi Oktoba 25, 2025 kuanzia saa 11:00 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Yanga inayoingia uwanjani ikiwa imetoka kufungwa bao 1-0 ugenini nchini Malawi, inahitaji ushindi wa angalau tofauti ya mabao 2-0 ili kufuzu hatua ya makundi kwa msimu wa nne mfululizo kwenye mashindano ya CAF baada ya 2022-2023 kufanya hivyo upande wa Kombe la Shirikisho Afrika, kisha 2023-2024 na 2024-2025 upande wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Moja ya viongozi, amefichua kwamba, kabla ya kuanza safari ya kurudi Dar es Salaam Jumatatu wiki hii, kulifanyika kikao kifupi na uongozi wa juu wa timu hiyo ukawanyooshea maneno wachezaji hasa wale nyota kama Maxi na Pacome kuwa, kuna ulazima kwao wachezaji kubadilika.

Yanga Presha Kubwa Kuelekea Kufuzu Makundi

Kwa mujibu wake, mabosi wa Yanga waliwaambia wachezaji hao kwamba, licha ya kumuondoa kocha Romain Folz, lakini hata wao wachezaji hawakucheza vizuri na mechi ya marudiano ipo kwenye mikono yao, lazima wafanye kweli wafuzu makundi.

β€œKumekuwa na vikao vya hapa na pale vya kuwakumbusha wachezaji nini wajibu wao kwenye timu na kipiΒ  wanatakiwa kufanya iliΒ  timu iweze kupata matokeo kesho.

β€œKwa sababu wenzetu wamekuja wakiwa na hamasa sana, kwahiyo kama hatutakaa vizuri, hali ineweza ikawa mbaya. Wapo wachezaji wale mastaa wamekumbushwa kujitoa zaidi,” alisema kiongozi huyo.

Juzi Jumanne mchana Oktoba 21, 2025, kikosi cha Yanga kiliingia kambini ikiwa ni baada ya Jumatatu Oktoba 20, 2025 kuwasili nchini kikitokea Malawi kilikochapwa bao 1-0 na Silver Strikers.

Bila kusahauΒ meridianbetΒ ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Yanga Presha Kubwa Kuelekea Kufuzu Makundi

Katika maandalizi ya mechi hiyo, kikosi cha Yanga hivi sasa kipo chini ya kocha Patrick Mabedi ambaye anakaimu nafasi ya Folz aliyeondoshwa muda mchache baada ya kupoteza mbele ya Silver Strikers.

Inafahamika kuwa, tangu kikosi hicho kiingie kambini, viongozi wamekuwa wakifanya vikao ikiwamo kujadili ujio wa kocha mpya na namna ya kukabiliana na Silver Strikers na kushinda Kwa Mkapa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.