Kamati ya Uendeshaji na usimamizi wa ligi ya bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Mei 19 2023, ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi na kufanya maamuzi yafuatayo juu ya Chama.

Ligi kuu ya NBC mechi namba 222: Simba dhidi ya Ruvu Shooting,
Mchezaji wa klabu ya Simba Cloutus Chota Chama amefungiwa michezo mitatu na faini ya laki 500,000 kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa klabu ya Ruvu Shooting, Abal Kassim Suleiman.
Tukio hilo lilitokea wakati wachezaji hao wawili wakigombea mpira, jambo ambalo lilifanya mwamuzi wa mchezo huo ashindwe kuona tukio hilo kwa haraka zaidi.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kanuni ya 41:5(5.2) ya ligi kuu kuhusu udhibiti kwa wachezaji.

Mchezo huo ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 huku kwa upande w aRuvu wao ndio mchezo ambao uliwafanya waage mashindano.

