Klabu ya Namungo FC ambayo ina makazi yake Lindi imemtambulisha Erasto Nyoni kama mchezaji wao mpya baada ya mchezaji huyo kuagwa na klabu ya Msimbazi jana.
Nyoni ambaye anacheza katika eneo la kiungo aliitumikia Simba takribani kwa miaka kadhaa mpaka jana ambapo jana aliachana rasmi na klabu hiyo huku akiweza kucheza kama kiungo na beki pia.
Licha ya kuitumikia klabu ya Simba Nyoni amekuwa hapati namba mara kwa mara klabuni hapo kutokana na umri na ushindani mkubwa uliyopo na hivyo mara nyingi kucheza kama mchezaji wa akiba.
Namungo inatarajia mchezaji huyo atatoa mchango mkubwa klabuni hapo kutokana na uzoefu wake mkubwa kwenye ligi kuu ya Tanzania na kuiwezesha timu hiyo kufika matarajio ambayo watayapanga kwa msimu ujao mpya.
Je Erasto anaenda kuwa mchango klabuni hapo msimu wa 2023/2024? na kwa kiasi gani ataonyesha kiwango chake na Wauaji wa Kusini?