Kwa mujibu wa Sky Sport Italia, Antonio Conte anachukua muda kidogo zaidi kuamua kuhusu mustakabali wake na Napoli baada ya mkutano muhimu uliofanyika jana na Rais Aurelio De Laurentiis.

Mkutano huo uliodumu takribani saa tatu pamoja na chakula cha mchana ulihudhuriwa na Rais De Laurentiis, kocha Conte, mke wake Elisabetta, mkurugenzi wa michezo Giovanni Manna, Mkurugenzi Mtendaji Maurizio Chiavelli na Makamu wa Rais Edoardo De Laurentiis.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Ulikuwa ukifanyika nyumbani kwa Rais huko Roma, baada ya wao na kikosi kizima cha Napoli kukutana na Papa Leo mjini Vatican.
Ingawa mkutano huo ulikuwa wa muda mrefu, ripoti nyingi zilikuwa tayari zimesema kuwa Conte alikuwa ameshaamua kuondoka Napoli, bila kujali mafanikio yao ya kushinda Scudetto.

Hata hivyo, hali hiyo sasa inaonekana kubadilika, kwani Sky Sport Italia wanaripoti kuwa pande zote mbili zimekubaliana kuchukua muda kabla ya kufanya uamuzi wowote wa mwisho.
Kuna shinikizo kubwa kwa Conte kubadili uamuzi wake na kubaki, ikiwemo kutoka kwa mkewe Elisabetta, ambaye alionekana akimwambia shabiki wakati wa gwaride la jana kwenye basi la wazi kuwa angefanya “kila liwezekanalo” kumshawishi abaki.
Romelu Lukaku pia alieleza vivyo hivyo, pamoja na wachezaji wengine, huku uwezekano wa kuwasili kwa Kevin De Bruyne kama mchezaji huru ukiwa wa kuvutia kwa kocha huyo.
Partenopei waliwapiku Inter kwa alama moja na kushinda taji la Serie A Ijumaa usiku, na wamekuwa wakisherehekea ushindi huo kwa gwaride kupitia mitaa ya Naples.



