Hali hii imebadilika haraka, kufuatia kikao kati ya Gasperini na viongozi wa Atalanta kilichofanyika Bergamo, kikao ambacho hakikuwa kimepangwa awali.
La Dea waliweka tarehe ya mwisho kwa Gasperini kutoa jibu kuhusu ofa ya mkataba mpya hadi Juni 2027, lakini badala yake aliwaambia kuwa hakuna kitu kingeweza kumbadilisha nia ya kuondoka baada ya miaka 9.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
Haikuwa kuhusu mshahara, wala mkakati wa usajili wa wachezaji, bali alihisi kuwa ameifikisha timu hiyo mbali kadri alivyoweza na sasa anatamani changamoto mpya.

Ripoti zinasema kuwa Gasperini yuko kwenye mawasiliano ya moja kwa moja na Roma kupitia Claudio Ranieri, na mambo yanaendelea kwa kasi huko pia.
Mtaalamu wa uhamisho wa Sportitalia, Alfredo Pedullà, anadai kuwa tangazo la kuondoka kwake Atalanta linaweza kutolewa mapema kama Jumatano asubuhi.
Pendekezo lililo mezani ni sawa na lile lililotolewa kwa kocha wa Como, Cesc Fabregas — mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya takriban €5 milioni kwa msimu, pamoja na bonasi.
Gasperini msimu huu akiwa Atalanta aemamaliza nafasi ya 3, nafasi ambayo itawafanya wacheze Ligi ya mabingwa msimu ujao, lakini pia walimaliza msimu kwa kupata kichapo wakiwa nyumbani.