Kiungo mshambuliaji mpya ndani ya kikosi cha Wydad Casablanca, Azizi Ki tayari ameanza mazoezi na timu hiyo mara baada ya kumtambulisha.

Ikumbukwe kwamba Ki aliibuka ndani ya timu hiyo akitokea kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.
Mechi kali leo hii Duniani zinaendelea na Meridianbet wapo tayari kuhakikisha hawakuachi hivyo hivyo, na ndio maana wameamua kukupatia ODDS za kibabe na machaguo zaidi ya 1000 kwenye mechi za leo.
Mchezo wa mwisho akiwa na uzi wa Yanga SC ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania ambao ulikuwa ni CRDB Federation Cup hatua ya nusu fainali.
Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga baada ya dakika 90 ubao ukasoma Yanga SC 2-0 JKT Tanzania.
Mei 25 Azizi Ki alitambulishwa rasmi ndani ya kikosi cha Wydad Casablanca kiungo huyo mshambuliaji ambaye alikuwa anavaa jezi namba 10 ndani ya kikosi cha Yanga SC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.

