Inatajwa kuwa kiungo wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga Azizi Ki huenda akasepa baada ya msimu wa 2024/25 kugota mwisho kwa kuwa amepata timu ambayo inahitaji huduma yake kutokana na uwezo alionao.

Ni Aziz Ki ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi kwenye eneo la kiungo akiwa ni mkali kwenye mapigo huru hasa penati na faulo ambapo kwa msimu huu Yanga ikiwa imepata penati 7 yeye alipewa jukumu kupiga sita.
Katika penati hizo ni nne alipata na mbili makipa waliokoa hatari hizo ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa KMC Complex na Tabora United uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Taarifa zinaeleza kuwa kuna timu moja kutoka Libya ambayo imefanya mawasiliano kwa ukaribu na mabosi wa Yanga na nyingine ni Kaizer Chiefs ambayo ilikuwa inahitaji saini ya Azizi Ki kwa muda mrefu.


