Ni Kama kazinduka kutoka kuzimu nyota Simba Kibu Denis ambaye jana alifunga kwa mara ya kwanza ndani ya ligi kuu baada ya kumaliza siku takribani 380 bila kuona bao.

Lakini Jana dhidi ya Dodoma Jiji aliweka chuma 2 na kutoa assist kwenye ushindi wa 6-0 dhidi ya Dodoma Jiji. Ni mbinu za Kocha Mkuu Fadlu Davids anayekinoa kikosi cha Simba zimejibu wakipata ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Dodoma Jiji mchezo wa Ligi Kuu Bara ikiwa ni mzunguko wa pili kwenye ligi namba nne kwa ubora Uwanja wa KMC, Complex.
Katika mchezo huo ni Ellie Mpanzu alifungua akaunti ya mabao dakika ya 15, Jean Ahoua akatupia mabao mawili dakika ya 21 na 45 huku Steven Mukwala akifunga bao moja dakika ya 47 akiwa ndani ya 18.
Kibu Denis alifunga dakika ya 54 kwa pigo la kichwa akiwa ndani ya 18 na bao la pili katupia dakika ya 69.
Ikumbukwe kwamba Kibu D mara ya mwisho kufunga kwenye ligi ilikuwa katika mchezo dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Novemba 5 2023. Yanga wakishinda 5-1.


