Mainoo Ahakikishiwa Nafasi Uwanjani Man United

Kobbie Mainoo ameonekana kushinda mapambano yake ndani ya Manchester United, huku kiungo huyu wa kimataifa wa Uingereza akikaribia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. Ilionekana kwa kipindi fulani kwamba maisha ya Mainoo yangeendelea nje ya Old Trafford, lakini mabadiliko ya kocha yameondoa mjadala huo wa uhamisho.

Mainoo alikosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza chini ya kocha wa zamani Ruben Amorim. Alianza mechi moja tu katika kampeni ya 2025-26 kwenye mchezo dhidi ya Grimsby Town ya Ligi daraja la Pili kabla ya kocha huyo wa Kireno kufutwa kazi. Hali hii ilimweka Mainoo kwenye ukingo wa kuondoka klabuni.

Mainoo Ahakikishiwa Nafasi Uwanjani Man United

Kuna ripoti kwamba klabu kadhaa barani Ulaya ikiwemo mabingwa wa Serie A, Napoli zingeweza kumchukua Mainoo ili apate dakika za kutosha za kucheza na kuendeleza kipaji chake. Hata hivyo, mikoba ya Manchester sasa ipo mikononi mwa kocha wa muda Michael Carrick, ambaye amemrejesha Mainoo kwenye kikosi cha kwanza. Kiungo huyo alicheza dakika zote 90 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Manchester City na alionyesha ubora wa hali ya juu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kulingana na Daily Mail, Manchester United sasa wanajiandaa kuanza tena mazungumzo nae ya mkataba. Masuala ya kuondoka yamesitishwa, huku mpango ukiwa ni kukihifadhi kipaji hiki kilichozaliwa Old Trafford. Ingawa mkataba wake wa sasa bado una miezi 18, una chaguo la kuongeza mwaka mmoja hadi 2028, jambo ambalo linaonyesha klabu inamhitaji Mainoo kwa muda mrefu.

Mainoo Ahakikishiwa Nafasi Uwanjani Man United

Chini ya Carrick, mchezaji huyo amepata nafasi ya heshima tena. Kocha huyu ambaye ni mchezaji wa zamani wa United alisema wazi kuwa ni shabiki mkubwa wa kipaji hicho: “Klabu ikiwa na mchezaji aliyetoka kwenye akademi na anaelewa utamaduni wa klabu, lazima ajumuishwe. Tunaona anaweza kuwa shina la timu,” Carrick alisema. Aidha, Carrick amemchambua kinda huyo siyo tu kama kiungo wa kuzuia, bali kama mchezaji wa kushambulia, anayehitaji uhuru kidogo zaidi ili kuonyesha uwezo wake kamili.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.